Text: | Mwokozi wangu umekosa nini |
Author: | J. Heermann, 1585-1647 |
1 Mwokozi wangu, umekosa nini?
Wahukumiwa kama mwuaji.
Umeshtakiwa makosa mangapi
uliyotenda?
2 Wapigwa sana, miiba taji lako,
umetemewa mate, watukanwa,
wanyweshwa nyongo,
tena siki kali, wasulibishwa!
3 Sababu gani unateswa hivi?
Makosa yangu yanakuumiza;
mateso haya yako yanipasa,
mimi mkosaji.
4 Ajabu kubwa sana tendo lako:
Mchungaji unateswa kwa ajili
ya kondoo, Bwana unawalipia
watumwa wako.
5 Tulipokuwa mateka ya mwovu,
nawe ukaja ukatukomboa.
Twalistahili kufa kwa milele,
ukatufia.
6 Mwokozi wangu nifanyeje mimi,
niitangaze pote sifa yako?
Nakufuata nikutumikie
maisha yote.
Text Information | |
---|---|
First Line: | Mwokozi wangu, umekosa nini? |
Title: | Mwokozi wangu umekosa nini |
German Title: | Herzliebster Jesu |
Author: | J. Heermann, 1585-1647 |
Language: | Swahili |
Publication Date: | 1988 |
Topic: | Kuteswa na kufa kwa Yesu |
Notes: | Sauti: Herzliebster Jesu, Asili: J. Crüger, 1598-1662, Posaunen Buch, Erster Band #133, Reichs Lieder #83, Tumwimbie Bwana #20, Service Book and Hymnal #421, Lutheran Book of Worship #123 |